Dr. Wilbroad P. Slaa
Dr. Wilbroad P. Slaa alikuwa ni Mtanzania wa pili kutunukiwa Tuzo ya MajiMaji ya Haki za Binadamu mwaka 2010, akiwa ni mtendaji (mbunge) kutoka mhimili wa Bunge. Dr. Wilbroad P. Slaa kutokana na kazi aliyoifanya bungeni kuanzia 2005 hadi 2010 kuisimamia serikali, kupambana na ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Alionyesha nia na uchu wa kudai uwajibikaji wa serekali kwenye mambo yenye nia ya kutetea, kulinda na kuendeleza Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini. Kwenye rekodi za majadiliano ya Bunge aliongoza kwa kutoa hoja nyingi, kuuliza maswali na kuchangia hoja mbalimbali kuliko wabunge wengine katika kipindi hicho.